Saturday 13 March 2010

Breaking News

Meli ya Serengeti maarufu kama mkombozi wa Pemba imeteketea vibaya kwa moto jioni ya leo huko katika bandari ya Zanzibar, meli hiyo ilikuwa ikijitayarisha kupakia abiria kwenda Pemba, wakati tukio hilo likitokea kulikuwa na mabaharia 8 ambao saba walijiokoa kwa kuogolea wenyewe na mmoja akibaki ndani ya meli kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa akijua kuogolea, hadi hivi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza kufahamika, kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wamesema moto ulianza katika chumba cha engine, juhudi ya fire kuuzima moto huo zilishindikana kutokana na kutokuwa na vifaa vya kuzima moto ndani ya bahari, mwaka jana pekee kulitokea ajali tatu za meli za mizigo na abiria kuwaka moto ambazo ni aziza one na two pamoja na meli ya MV Pemba

Bidhaa Bei Juu bado

Licha ya umeme kurudi bado bidhaa mbalimbali ambazo zilipanda ikiwa sababu ni umeme hazijashuka, baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji kwa mfano chupa ya ujazo wa lita moja na nusu kabla ya kukatika umeme ilikuwa inauzwa kwa shilingi 600 hadi 700 kipindi cha kukatwa kwa umeme chupa hiyo ilipanda hadi 1000 kw a kisingizio cha kutumia gharama zaidi ya mafuta ya generator, kujaza upepo kwa tairi la gari kabla ya kukatika umeme ilikuwa 100 hadi 200 kipindi cha kiza ikawa 500, kuziba puncha kabla ilikuwa 500 kipindi cha umeme 2500 hadi 4000, na nyingi nyenginezo hata hivyo licha ya umeme kurudi bei ya bidhaa hizo zimebaki vilevile

Umeme Bado baadhi ya sehemu

Licha ya umeme kurejeshwa tarehe 8 mwezi huu bado kuna maeneo hadi hii leo hawajapata umeme, baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na ya mjini ambapo katika kile cha kushangaza utakuta nyumba ya jirani kuna umeme na inayofuata haina umeme, kwa mfano hadi leo baadhi ya nyumba chukwani hawana umeme, mtoni, vikokotoni na sehemu za ngambu halikadhalika, hata hivyo shirika la umeme limewataka wale wote ambao hawapati umeme kwenda kutoa taarifa, wakati umeme ukiwa umerudi kumekuwepo na kukatikakatika kwa umeme huo mara kwa mara kwa bila ya kutolewa taarifa rasmi huku ikiwacha watu wakiwa na wasiwasi na kutilia shaka umeme huo.

Tuesday 9 March 2010

UMEME WARUDI ZANZIBAR

Hatimae baada ya miezi mitatu umeme warejea tena Zanzibar tokea ulipokatika tarehe 10 Decemba mwaka jana. umeme huo umerejea kwa sehemu kubwa ya Zanzibar huku maeneo mengine yakiachwa bila ya umeme kutokana na sababu za kuibiwa waya pamoja na kuharibika kwa transfoma. wananchi wazanzibar wamepokea kwa furaha kurejea kwa umeme baada ya kuka kwa kipindi chote hicho bila ya umeme na kuyafanya maisha yao kuwa magumu.