Saturday, 13 March 2010

Breaking News

Meli ya Serengeti maarufu kama mkombozi wa Pemba imeteketea vibaya kwa moto jioni ya leo huko katika bandari ya Zanzibar, meli hiyo ilikuwa ikijitayarisha kupakia abiria kwenda Pemba, wakati tukio hilo likitokea kulikuwa na mabaharia 8 ambao saba walijiokoa kwa kuogolea wenyewe na mmoja akibaki ndani ya meli kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa akijua kuogolea, hadi hivi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza kufahamika, kwa mujibu wa mashuhuda wa moto huo wamesema moto ulianza katika chumba cha engine, juhudi ya fire kuuzima moto huo zilishindikana kutokana na kutokuwa na vifaa vya kuzima moto ndani ya bahari, mwaka jana pekee kulitokea ajali tatu za meli za mizigo na abiria kuwaka moto ambazo ni aziza one na two pamoja na meli ya MV Pemba

Bidhaa Bei Juu bado

Licha ya umeme kurudi bado bidhaa mbalimbali ambazo zilipanda ikiwa sababu ni umeme hazijashuka, baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji kwa mfano chupa ya ujazo wa lita moja na nusu kabla ya kukatika umeme ilikuwa inauzwa kwa shilingi 600 hadi 700 kipindi cha kukatwa kwa umeme chupa hiyo ilipanda hadi 1000 kw a kisingizio cha kutumia gharama zaidi ya mafuta ya generator, kujaza upepo kwa tairi la gari kabla ya kukatika umeme ilikuwa 100 hadi 200 kipindi cha kiza ikawa 500, kuziba puncha kabla ilikuwa 500 kipindi cha umeme 2500 hadi 4000, na nyingi nyenginezo hata hivyo licha ya umeme kurudi bei ya bidhaa hizo zimebaki vilevile

Umeme Bado baadhi ya sehemu

Licha ya umeme kurejeshwa tarehe 8 mwezi huu bado kuna maeneo hadi hii leo hawajapata umeme, baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na ya mjini ambapo katika kile cha kushangaza utakuta nyumba ya jirani kuna umeme na inayofuata haina umeme, kwa mfano hadi leo baadhi ya nyumba chukwani hawana umeme, mtoni, vikokotoni na sehemu za ngambu halikadhalika, hata hivyo shirika la umeme limewataka wale wote ambao hawapati umeme kwenda kutoa taarifa, wakati umeme ukiwa umerudi kumekuwepo na kukatikakatika kwa umeme huo mara kwa mara kwa bila ya kutolewa taarifa rasmi huku ikiwacha watu wakiwa na wasiwasi na kutilia shaka umeme huo.

Tuesday, 9 March 2010

UMEME WARUDI ZANZIBAR

Hatimae baada ya miezi mitatu umeme warejea tena Zanzibar tokea ulipokatika tarehe 10 Decemba mwaka jana. umeme huo umerejea kwa sehemu kubwa ya Zanzibar huku maeneo mengine yakiachwa bila ya umeme kutokana na sababu za kuibiwa waya pamoja na kuharibika kwa transfoma. wananchi wazanzibar wamepokea kwa furaha kurejea kwa umeme baada ya kuka kwa kipindi chote hicho bila ya umeme na kuyafanya maisha yao kuwa magumu.

Monday, 22 February 2010

DNA Bado Kitendawili Zanzibar

Wizara ya afya na ustawi wa jamii Zanzibar imesema imeshatafuta Mtaalamu maalum watakao fanya utafiti juu ya kuwepo kipimo cha DNA nchini ili kuondosha usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa kipimo hicho. Katibu mkuu wizara ya Afya na ustawi wa Jamii Zanzibar Mohammed Saleh Jidawi amesema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa kitengocha hifadhi ya mtoto iliyozinduliwa katika hoeli ya zanzibar ocen view kilimani mjini zanzibar. ….CLIP(SAVED-JIDAWI). Aidha ametoa wito kuwepo kwa ushirikiano na taasisi mbali mbali nchini pamoja washirika wa maendeleo kushirikiana katika utoaji wa elimu kwa wanachi juu ya haki za watoto.
Nae katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali Mwanaidi Saleh ameitaka jamii kubadilika na kuelekeza nguvu zao katika kutokomeza tatizo la ubakaji …..CLIP(SAVED-WEMA)
Aidha amekitaka kitengo hicho cha uhifadhi wa watoto kuandaa muongozo maalum wa kitaifa ili kuendeleza ustawi wa watoto.\ Na Zenj fm

Wastaafu Watakiwa Kuwapisha Vijana Zanzibar

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kuachana na mpango wa kuwaongezea muda watumishi wake wanaostaafu hatua ambayo itawasaidia vijana kupata nafasi za ajira. Mwenyekiti wa chama cha siasa cha AFP Said Soud Said amesema vijana wengi wanaomaliza masomo yao wanakosa nafasi za ajira serikalini kwa kisingizio cha kukosa uzowefu. Amesema endapo serikali itaendelea na mpango huo, taifa litabeba mzigo mkubwa kutokana na baadhi ya vijana kujihusisha na vitendo viovu wakati wanapokosa ajira. Hata hivyo amesema baadhi ya wafanyakazi wanastahiki kuongezewa muda kama vile madaktari, lakini sio kwa taasisi nyingine. ……CLISP…(SAVED-SAID

kwa hisani ya Zenj Fm

Asilimia 54 Wajiandikisha Kupiga Kura Zbar Awamu ya Kwanza

Jumla ya wapiga kura wapya laki mbili na elfu 71, 376 wamejiandikisha katika daftari la wapiga kura Zanzibar kwa awamu ya kwanza iliyoanza mwaka jana hadi Februari 14 mwaka huu.
Kwa mujibu wa takwimu za tume ya uchaguzi Zanzibar undikishaji huo umepata mafanikio kwa asilimia 53.50 ikilinganishwa na unadikishaji wa wapiga kura uliofanyika mwaka 2005 ambapo tume hiyo ilisajili wapiga kura wapya laki mbili, elfu 35, 849.Kazi za uandikishaji ambazo kwa sasa zimo katika matayarisho kwa awamu ya pili, tume ya uchaguzi imekadiria kuandikisha zaidi ya asilimia 46.50 ya wapiga kura kwa Unguja na Pemba.Katika uandikishaji huo wa awamu ya kwanza ya wapiga kura wapya Kisiwa cha Unguja kimeonesha kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura waliofikia laki mbili, elfu tisa na 49 wakati Pemba watu waliojiandikisha ni elfu 63, mia tatu na 27.

Habari kwa hisani ya Zenj Fm Zanzibar

Thursday, 18 February 2010

Mswada kwa ajili ya mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi waiva

Serikali ya Zanzibar inatarajiwa kupeleka mswada utakaopelekea kufanyiwa marekebisho sheria ya uchaguzi ili kuruhusu tume ya uchaguzi kusimamia zoezi la kura za maoni, mswada huo unatarajiwa kupelekwa katika baraza la Wawakilishi mwezi ujao, mwanasheria mkuu wa Serikali Iddi Pandu Hassan amedhibitisha kuwa mswada upo tayari na tayari ushapelekwa katika baraza la mapinduzi kwa hatua zaidi. kufanyika kwa kura`za maoni kutapelekea uundwaji wa serikali ya mseto au kuendelea kwa mfumo wa serikali uliokwepo hivi sasa kulingana na maoni ya wananchi.