Wednesday, 17 February 2010

CCM Yaridhia Maridhiano Zanzibar

Kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM imepitisha kwa sauti moja kusudio la Baraza la Wawakilishi Zanzibar la kutaka kuundwa kwa Serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar, katika azimio lake CCM imeitaka SMZ mara moja kupeleka mswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi Zanzibar, lengo la kupeleka mswada huo ni kuhakikisha tume ya uchaguzi ya Zanzibar inapatiwa jukumu la kusimamia na kuandaa kura za maoni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu. Halmashauri kuu ya CCM pia imetangaza mwezi Julai ndo utakuwa mwezi wa kuchukua fomu kwa wale wanaotaka kugombea uwakilishi, ubunge, Urais wa Zanzibar na ule wa Muungano. Hata hivyo wamesema ni ruhusa kwa mtu yeyote anayetaka kuonyesha nia ya kugombea nafasi hizo kuonyesha ila asianze kufanya kampeni mapema

No comments: