Sunday, 14 February 2010
Viwavi Jeshi Vyaathiri Kilimo Zbar
Wimbi la viwavi jeshi vilivyosambaa sehemu mbalimbali za kilimo Zanzibar vimeathiri kwa kiasi kikubwa kilimo na kupelekea hofu ya kuwepo upungufu wa chakula Zanzibar. viwavi jeshi jeshi hivyo vimeathiri zaidi katika mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na Mkoani Pemba, katika eneo moja tu Mkoani vimeathiri shamba la mpunga lenye ukubwa wa heka 23, Wizara ya Kilimo na mifugo Zanzibar imeahidi kusaidia kuwangamiza viwavi jeshi hao ambao hivi sasa wanaonekana kuwa ni tatizo kubwa kwa wakulima Zanzibar, nchi ya Zanzibar licha ya kuwa na wataalamu kadhaa wa kilimo bado kilimo hakijafanikiwa na asilimia kubwa ya wakulima wanatumia jembe la mkono.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment