Friday, 12 February 2010

Kuku sasa Ruhusa Kuingizwa Zanzibar

Serikali ya Zanzibar imetoa tamko rasmi la kuruhusu uingizaji wa kuku na jamii ya ndege kutoka sehemu yeyote ulimwenguni kuanzia sasa hivi. Tamko hilo la serikali limetolewa na Waziri anayehusika na mambo ya mifugo Zanzibar Burhan Saadat baada ya kupigwa marufuku kufuatia ugonjwa wa mafua ya ndege, amesema hivi sasa hali inaonekana kuwa ni shwari na ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa umedhibitiwa ulimwenguni. Mapema mwaka jana Serikali ilipiga marufuku uingizaji wa kuku na jamii ya ndege kufuatia kuibuka kwa maradhi hayo kitu ambacho kilipelekea kuongezeka marudufu bei ya kuku ambapo robo kuku na chips hivi sasa ni 5000! ambapo familia yenye watoto wawili baba na mama wakitaka kula kuku chips kwa wakati mmoja inawalazimu kutumia 20000 kwa wakati mmoja ikiwa ni robo ya mshahara wa kiwango cha chini.

No comments: