Friday, 12 February 2010
Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kukamilika Agost mwaka huu
Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Zanzibar unaoendelea kutengezwa umefikia hatua ya asilimia 50. ujenzi huo uliaoanza kujengwa April 17 mwaka jana na kampuni ya Kifaransa inayoitwa Sogea Satom Vinci unatakiwa kukamilika Ogasti mwaka huu. kukamilika kwa ujenzi huo kutapelekea ndege kubwa kuweza kutua moja kwa moja Zanzibar, tofauti ilivyo hivi sasa kwa ndege kubwa kutuwa Tanzania Bara isipokuwa Ethiopian Airline na hivyo kupelekea usumbufu kwa abiria wanaotaka kusafiri moja kwa moja Zanzibar kutoka nchi za nje, Meneja Mkuu wa mradi huo wa njia ya kurukia ndege uwanjani hapo Nichel Bescher ameahidi kazi hiyo kukamilika kwa muda muwafaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment