Thursday, 11 February 2010
Zanzibar Kuendelea kuwepo Kizani hadi March
Kisiwa cha Unguja kitaendelea kuwepo kizani tena kwa mwezi mmoja kufuatia mafundi kutokamilisha kazi za ufungaji wa vifaa vipya unaondelea hivi sasa. Awali kwa mujibu wa ratiba ya mwanzo umeme ulipaswa kurudi tarehe 20 ya mwezi huu wa Februari. Hata hivyo kwa sababu ambazo hadi sasa hazijawekwa wazi na kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mafundi wanaotengeza umeme hivi sasa zoezi la kukamilisha ufungaji wa umeme litamaliza tarehe 25 hadi 27 Februari mwaka huu. kwa maana hiyo kutokana na kuwa mwezi huu unaishia tarehe 28 ndo kusema umeme unatarajiwa kurudi mwezi ujao wa March. Tokea tarehe 10 Desemba ya mwaka jana Zanzibar ipo kizani kufuatia kuharibika kwa njia kuu ya kuleta umeme kutoka bara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment