Thursday, 11 February 2010

Gurnah-Mzanzibar Aliyetoka katika ukimbizi hadi Uprofesa Uengereza

Kwa hapa Zanzibar bila shaka kwa vijana wakawaida inaweza kuwa jina la Gurnah kwao wao si lolote wa s chochote, wengi ukiwambia unamfaham Abdulrazak Gurnah watakuliza ni nani na anaka wapi, lakini ulimwenguni jina la Gurnah ni maarufu mno. Na umaarufu wake umezidi hata mipaka ya kawaida, umaarufu huo haukutokana tu kwa kuwa Gurnah bali kutokana na umahiri wake katika lugha ya kiengereza na utunzi wa vitabu, Gurnah kwa hivi sasa ni Profesa wa lugha anayesomesha katika chuo kikuu cha Kent kilichopo London Uengereza, alizaliwa Zanzibar ambapo akiwa na umri wa miaka 17 alikimbia Zanzibar na Kwenda Uengereza kwa lengo la kujiendeleza, aliondoka Zanzibar mwaka 1965 ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na mwaka mmoja baada ya Muuongano na iliyokuwa Tanganyika, wakati ambapo fursa za kielimu zilikuwa haba kutokana na kuwepo na chuo kikuu kimoja tu maarufu Afrika Mashariki ambapo watuwalikuwa wakikitegmea ambacho ni Makerere, kwa vile aliondoka kimipangomipango alikupangana na changamoto kadha wa kadha zikiwemo za ubaguzi nchini Uengereza, akiwa hapo uengereza licha ya changamoto hizo aliamua kujiendeleza na hadi kuwa Profesa pengine unaweza kusema ni maarufu kuliko wanasiasa wengi nchini humo, umaarufu wake hautokani eti alikuwa mkimbizi bali unatokana na uwezo wake na tuzo anazopata za utungaji wa vitabu bora ulimwenguni, akiwa nchini humo alioa mzungu ambaye anaendelea kuishi naye hadi sasa, Gurnah baada ya safari yake refu ya ukimbizi kwa mara ya kwanza alirejea zanzibar kutembelea akiwa na umri wa miaka 32 mwaka 1980, hivi sasa Abdulrazak Gurnah ana umri wa miaka 62 ambapo zaidi ya asilimia 80 ya umri wake akiwa ameishi ugenini kw amaana ya kwamba miaka 45 ameishi Uengereza na 17 tu ndio aliyoishi alpozaliwa Zanzibar kuliko na familia yake kubwa.

No comments: